Wapendwa wanafamilia ya Mungu, katika kikao cha kwanza cha kamati kuu ya maandalizi ya Sinodi, Baba Askofu Michael Msonganzila aliweka wazi sababu tisa zinazotufanya tuadhimishe Sinodi wakati huu. Tunapenda sasa wasomaji wetu wapendwa wazifahamu sababu hizi muhimu kwetu katika kuadhimisha Sinodi ya Jimbo letu la Musoma.
Ratiba na Maelekezo Muhimu
Thursday, November 1, 2012
Wednesday, September 5, 2012
Takwimu za Jimbo la Musoma
Endapo unapenda kuzifahamu takwimu muhimu za Jimbo la Musoma, uitembelee tovuti ya Catholic Hierarchy inayokusanya takwimu zote za Maaskofu na Majimbo ya dunia nzima. Ukurasa unaohusu Jimbo letu la Musoma unapatikana hapa. Katika ukurasa huo utapata habari za historia ya Jimbo, taarifa za Maaskofu wote walioongoza Jimbo letu, takwimu za waamini, anuani na kadhalika. Ifahamu Jimbo lako la Musoma!
Sehemu ya ukurasa wa Jimbo la Musoma katika tovuti ya Catholic Hierarchy |
Moyo wa Jimbo la Musoma
Mahali Jimbo la Musoma lilipozaliwa mnamo tarehe 3 Oktoba 1957 - siku Askofu wa kwanza wa Jimbo, Mhashamu John James Rudin, alipowekwa wakfu kuwa Askofu |
Patakatifu pa Kanisa Kuu la Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, Musoma mjini |
Altare ya Somo wa Kanisa Kuu na Jimbo - Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu |
Tabernakulo ya Kanisa Kuu la Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, Musoma mjini |
Mwongozo wa Sinodi ya Kijimbo
Katika mkutano wa kwanza wa kamati kuu ya maandalizi ya Sinodi ya Jimbo la Musoma, Mhashamu Baba Askofu Michael Msonganzila alidokeza kuwepo kwa hati ihusuyo Mwongozo wa Sinodi ya Kijimbo iliyotolewa mwaka 1997 na Idara ya Maaskofu (Congregation for Bishops) pamoja na Idara ya Uinjilishaji wa Mataifa (Congregation for the Evangelization of Peoples) ya Vatikano. Baba Askofu alitaka wajumbe wa kamati kuu waifahamu hati hii na kuitumia katika kazi za kamati.
Kwa kurahisisha usambazaji wa hati hiyo iitwayo 'Instruction on Diocesan Synods', kwa wajumbe wa kamati kuu pamoja na waamini wote wa Jimbo letu la Musoma, tunawaleteeni anuani ya tovuti ya Vatikano, hati hiyo inapopatikana 'online'. Kupata hati hiyo kamili, tafadhali bofya hapa ama uibofye linki ya mwongozo upande wa kulia wa blogu hii katika sura ya Important Links.
Tunawatakia usomaji mwema! Tunatumaini mwongozo huo utatusaidia sote kwenda pamoja katika kufanikisha Sinodi yetu.

Mwongozo wa Sinodi za Kijimbo unavyoonekana katika tovuti ya Vatikano |
Monday, September 3, 2012
Mkutano wa Kwanza wa Kamati Kuu ya Sinodi ya Jimbo
Mhashamu Baba Askofu Michael Msonganzila siku ya Upadrisho wa Mapadre wapya wawili - Benedicto Luzangi na Constantine Changwe - alitangaza nia yake ya kuadhimisha Sinodi ya Jimbo la Musoma kuanzia mwaka wa 2013 hadi 2014. Aidha, alitangaza kamati kuu ya Sinodi ya Jimbo yenye wajumbe wapatao 28 chini ya uenyekiti wa Mhe. Pd. Robert Luvakubandi, Paroko wa Kanisa Kuu la Musoma mjini.
Mkutano wa kwanza wa kamati ulipangwa tarehe 28 Agosti 2012 katika ukumbi wa mikutano wa Conference Center Musoma mjini. Na ndivyo ilivyokuwa. Wajumbe wa kamati walihudhuria mkutano na mambo muhimu kadhaa ya kimsingi yalizungumzwa kwa kina, kamati ndogondogo zikateuliwa na wajumbe waliweka dira ya kazi za kamati hadi mkutano wa pili utakaofanyika mwishoni mwa mwezi wa Oktoba mwaka huu.
Kamati Kuu ya Sinodi inaowaomba wanajimbo wote na watu wote wenye mapenzi mema waziombee kazi za kamati, waiombee Sinodi ya Jimbo na kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa Sinodi.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, Somo wa Jimbo la Musoma, utuombee!

Mkutano wa kwanza wa Kamati Kuu |
Subscribe to:
Posts (Atom)