Mwongozo wa Sinodi

RATIBA YA MATUKIO

· 21 – 22 Januari 2013: Semina kwa wajumbe wa Sinodi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwembeni, Musoma.

· Januari – Mei 2013: Kuhamasisha na kutoa mafundisho kuhusu Sinodi; kukusanya maoni na mapendekezo kwa watu wote wa Taifa la Mungu jimboni Musoma.

· 19 Mei 2013: UZINDUZI RASMI WA SINODI. Adhimisho la Misa Takatifu ya Sherehe ya Pentekoste katika Kanisa Kuu la Jimbo.

· 03 – 07 Juni 2013: Awamu ya Kwanza ya Vikao vya Sinodi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwembeni, Musoma.

· 09 – 13 Desemba 2013: Awamu ya Pili ya Vikao vya Sinodi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwembeni, Musoma.

· 28 Aprili – 02 Mei 2014: Awamu ya Tatu ya Vikao vya Sinodi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwembeni, Musoma.

· 04 – 08 Agosti 2 014: Awamu ya Nne ya Vikao vya Sinodi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwembeni, Musoma.

· Agosti – Oktoba 2014: Sekretarieti na kamati ya Mawasiliano kuchapa Matamko na Maazimio

· 03 Oktoba 2014: KUHITIMISHA SINODI. Adhimisho la Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Jimbo.


UWAKILISHI KATIKA VIKAO VYA SINODI
1. Mapadre wote
2. Wawakilishi wa nyumba za kitawa zilizomo jimboni
3. Wajumbe wa Kamati Kuu ya Sinodi
4. Wawakilishi wawili toka kila parokia
5. Gombera wa Seminari, Walezi nyumba za malezi
6. Makamu wa Askofu katika sheria, Watawa
7. Wawakilishi vyama vya Kitume na Makundi Maalumu.
8. Ex officio wengine kadiri ya mwono wa Askofu (Nafasi tatu)

Jumla ya wajumbe wote wa Sinodi inategemewa kuwa watu 170.

WATAALAMU WAWEZESHAJI WA SEMINA 
1. Padre Romwald Kajala – Jimbo la Rulenge-Ngara (0787181028)
 2. Padre Dr. Laurenti Magesa Cornelli


MGAWANYO WA MADA ZA KUZUNGUNZIA KATIKA VIKAO VYA MIJADALA YA SINODI NGAZI YA JIMBO

KIKAO CHA KWANZA: Tarehe 03 hadi 07 June 2013
Mada:  UINJILISHAJI WA IMANI NA CHANGAMOTO ZA NYAKATI ZETU, MIITO NA CHANGAMOTO ZA WAKATI.
A. Katekesi: Elimu ya dini shule za msingi, sekondari na vyuo, mafundisho ya msingi ya imani Katoliki.

B. Ufundishaji wa Dini
i. Mwongozo wa Mafundisho ya Dini:
ii. Mitaala
iii. Maandalizi ya waalimu wa dini, Makatekista n.k.
iv. Malezi endelevu na maisha ya sala kwa waamini

C. Maisha ya Sakramenti:
i. Ubatizo
ii. Ekaristi Takatifu
iii. Kipaimara
iv. Kitubio
v. Mpako wa wagonjwa
vi. Upadre
vii. Ndoa

D. Vyama vya Kitume:
i. Tume mbalimbali za wana wa Mungu kupitia vyama hivi vya kitume Utume wa Watoto (Utoto Mtakatifu), Utume wa Vijana (TYCS na VIWAWA), WITO, UWAKA, WAWATA, Wanandoa (Marriage Encounter) na wa Wazee, na vyama vingine vinavyokuza moyo wa ibada
ii. Utume wa Biblia
iii. Karismatiki/Uamusho na changamoto za kichungaji
iv. Vyama vingine vinavyoibuka na ibada zinazoambatana navyo.
v. Moyo wa Yesu, Mt. Alois, Mt. Vincent wa Paulo, utume wa sala, Legio ya Maria n.k.

E. Jumuiya Ndogondogo:
i. Malezi bora ya familia za Kikristo:

F. Wadau wa Uinjilishaji: Nafasi zao katika uinjilishaji na mahusiano wao.
i. Mapadre,
ii. Watawa,
iii. Makatekista
iv. Halmashauri mbalimbali, na vyama vya kitume.

G. Taasisi za Kanisa na Uinjilishaji:
i. Mashule na vyuo
ii. Hospitali, vituo vya afya na zahanati
iii. Taasisi zingine
iv. Uinjilishaji wa makundi maalumu: wakimbizi, wafungwa, wagonjwa, watalii,walemavu, migodini, wasafiri n.k.

H. Miito
i. Hali halisi ya miito katika Kanisa ulimwengu na Kanisa mahalia.
ii. Mchango wa mashirika ya Kimisionari katika kukuza miito ya Upadre na Utawa
- Mapadre na watawa wa Jimbo
- Mapadre na watawa wa mashirika yasiyo ya kijimbo
iii. Seminari ndogo, Nyumba za Malezi na Vyama vya Miito:
iv. Wadau wa malezi ya miito: wajibu wao katika malezi.
v. Changamoto za miito na namna ya kukabiliana nazo.

I. Changamoto za sasa katika uinjilishaji: utandawazi, ushirikina, kuibuka kwa madhehebu lukuki n.k



KIKAO CHA PILI: tarehe 09 hadi 13 December 2013

Mada:  LITURJIA YA KANISA NA MAISHA YA SAKRAMENTI
Madhehebu (Rites)
A. Maana na umuhimu wa Liturjia Katoliki

B. Misa Takatifu, heshima Kanisani na wakati wa maadhimisho ya kiliturjia.

C. Ibada ya Jumapili bila Padre:

D.. Mfumo wa mapadre katika maadhimisho ya Misa, usawa katika maadhimisho.

E. Nafasi ya visakramenti katika liturjia na matumizi yake kwa jumla.

F. Utamadunisho,
i. Nafasi ya utoto mtakatifu katika kutamadunisha liturjia.

G. Muziki na nafasi ya kwaya na nyimbo za kiliturjia.

H. Ibada ya Mazishi na wanaostahili kuzikwa kikristo

I. Mila na desturi za makabila zinazopingana na ukristo

J. Ibada za Karismatiki

K. Upungaji pepo, wenye idhini ya Kanisa katika kufanya utume huo

L. Changamoto za sasa katika maadhimisho ya kiliturjia

M. Ibada mpya ya maadhimisho wa liturjia


KIKAO CHA TATU: tarehe 28 Aprili hadi 025 Mei 2014
Mada:  UTUME WA HAKI AMANI NA UPATANISHO
A. Mahusiano
i. Mahusiano baina ya Wakatoliki jimboni. Askofu, Mapadre, watawa, waamini walei. Mahusiano na halmashauri mbalimbali na vyama vya kutume, makatekista.
ii. Mahusiano na madhehebu mengine ya Kikristo.
iii. Mahusiano na dini zisizo za kikristo [waislamu na dini za jadi].

B. Haki, Amani na Maridhiano
i. Mafundisho ya Kanisa kuhusu jamii
ii. Ukeketaji na tohara za kienyeji
iii. Utekelezaji wa sinodi ya pili ya Afrika
iv. Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania: wajibu na haki za raia
v. Wajibu na haki za watumishi jimboni

KIKAO CHA NNE: Tarehe 04 hadi 08 Agosti 2014
Mada: MAENDELEO NA KUJITEGEMEA

A. Huduma za Jamii: elimu, afya, maji safi, umeme na miundombinu

B. Rasilimali watu (Personnel): Posho/mishahara, mikataba na maslahi ya wahudumu mbalimbali wa Kanisa

C. Vyanzo vya mapato na udhibiti mali na mapato

D. Uwajibikaji na uwazi katika umiliki na matumizi ya mali ya Kanisa.

E. Mawasiliano kama hatua ya maendelea katika Kanisa

F. Changamoto za maendeleo
i. Kero za Kesi za Ardhi na kutotunza ardhi za taasisi zetu.
ii. Matumizi ya mali za zilizopo za Kanisa, kubadiri matumizi ya mali na vituo vya huduma.
iii. Uhifadhi wa mazingira.


SINODI MUSOMA - IMANI NA MATENDO










No comments: