Monday, September 3, 2012

Mkutano wa Kwanza wa Kamati Kuu ya Sinodi ya Jimbo

Mhashamu Baba Askofu Michael Msonganzila siku ya Upadrisho wa Mapadre wapya wawili - Benedicto Luzangi na Constantine Changwe - alitangaza nia yake ya kuadhimisha Sinodi ya Jimbo la Musoma kuanzia mwaka wa 2013 hadi 2014. Aidha, alitangaza kamati kuu ya Sinodi ya Jimbo yenye wajumbe wapatao 28 chini ya uenyekiti wa Mhe. Pd. Robert Luvakubandi, Paroko wa Kanisa Kuu la Musoma mjini.

Mkutano wa kwanza wa kamati ulipangwa tarehe 28 Agosti 2012 katika ukumbi wa mikutano wa Conference Center Musoma mjini. Na ndivyo ilivyokuwa. Wajumbe wa kamati walihudhuria mkutano na mambo muhimu kadhaa ya kimsingi yalizungumzwa kwa kina, kamati ndogondogo zikateuliwa na wajumbe waliweka dira ya kazi za kamati hadi mkutano wa pili utakaofanyika mwishoni mwa mwezi wa Oktoba mwaka huu.

Kamati Kuu ya Sinodi inaowaomba wanajimbo wote na watu wote wenye mapenzi mema waziombee kazi za kamati, waiombee Sinodi ya Jimbo na kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa Sinodi.

Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, Somo wa Jimbo la Musoma, utuombee!

Mkutano wa kwanza wa Kamati Kuu

No comments: