Wednesday, September 5, 2012

Mwongozo wa Sinodi ya Kijimbo

Katika mkutano wa kwanza wa kamati kuu ya maandalizi ya Sinodi ya Jimbo la Musoma, Mhashamu Baba Askofu Michael Msonganzila alidokeza kuwepo kwa hati ihusuyo Mwongozo wa Sinodi ya Kijimbo iliyotolewa mwaka 1997 na Idara ya Maaskofu (Congregation for Bishops) pamoja na Idara ya Uinjilishaji wa Mataifa (Congregation for the Evangelization of Peoples) ya Vatikano. Baba Askofu alitaka wajumbe wa kamati kuu waifahamu hati hii na kuitumia katika kazi za kamati.

Kwa kurahisisha usambazaji wa hati hiyo iitwayo 'Instruction on Diocesan Synods', kwa wajumbe wa kamati kuu pamoja na waamini wote wa Jimbo letu la Musoma, tunawaleteeni anuani ya tovuti ya Vatikano, hati hiyo inapopatikana 'online'. Kupata hati hiyo kamili, tafadhali bofya hapa ama uibofye linki ya mwongozo upande wa kulia wa blogu hii katika sura ya Important Links.

Tunawatakia usomaji mwema! Tunatumaini mwongozo huo utatusaidia sote kwenda pamoja katika kufanikisha Sinodi yetu.

Mwongozo wa Sinodi za Kijimbo
unavyoonekana katika tovuti ya Vatikano

No comments: