Friday, May 10, 2013

MAANDALIZI YA UFUNGUZI YAPAMBA MOTO

Kuelekea tukio la ufunguzi wa Sinodi ya Jimbo la Musoma, maandalizi yazidi kupamba moto ili tukio hilo liweze kufana. Waamini kote Jimboni wanasubiri kwa hamu tukio hilo la kihistoria na lenye umuhimu wa pekee katika maisha na ustawi wa Jimbo.

Akielezea maandalizi hayo mapema leo, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Sinodi, Mhe. Pd. Robert Luvakubandi alisema kuwa tayari Baba Askofu ameshatoa barua ya kutangaza ufunguzi rasmi wa Sinodi. Ufunguzi huo utafanyika siku ya Pentekoste tarehe 19 Mei mwaka huu 2013 katika viwanja vya Matumaini Katika Vijana. “Maelekezo maalumu pia yametolewa kwa maparoko kuwaandaa waamini kushiriki kikamilifu katika tukio hili” aliongeza Pd. Luvakubandi ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Musoma Mjini.

Aidha, Pd. Luvakubandi aliainisha kamati mbalimbali zilizoundwa kuandaa na kutoa huduma mbalimbali siku hiyo. Nazo ni Kamati ya Liturjia chini ya uenyekiti wa Pd. Benedict Luzangi, Kamati ya Usafi wa Mazingira, Jukwaa, Maturubai na Viti chini ya Uenyekiti wa Pd. Jeremiah Musira na Kamati ya Chakula na Vinywaji chini ya Uenyekiti wa Pd. Julius Magere.

Nyingine ni Kamati ya Afya chini ya Sr. Anastazia Salla CDNK na Sr. Bernadeta Beda IHSA, Kamati ya Fedha chini ya Pd. Leo Kazeri na Kamati ya Ulizi chini ya Nd. Egid Kilosa.

Kamati ya Liturjia itawajumuisha pia Sr. Winifrida Nyafuru IHSA (Katibu) na wajumbe Mnovisi Elizabeti Saka, Mnovisi Yasinta Cosmas, Shemasi William Bahitwa, Kat. Fredrik Raymond na Kat.Thomas Shagga. Wajumbe wengine wa kamati hii ni Mwl. Sospeter Chacha, Ms. Regina, Stella Dunia, Generose Mujuni na Mrs. Lucas Hupa.

Katibu wa kamati ya Usafi, Jukwaa, Maturubai na Viti ametajwa kuwa ni Br. Masini Kaswamila. Wajumbe wa Kamati hiyo ni Pd. Pius Msereti, Victor Mujuni, Maria Aloyce na Deogratias Nyantira.

Kamati ya Chakula na Vinywaji itawajumuisha Sr. Rose Aloyse (Katibu) na wajumbe Ma. Restituta Lukona, Monica James, Mwl. Maryness Martine na Nd. John Mkombozi.

Ms. Liz Mach na Nd. Archard Rwamunwa watakuwa katika Kamati ya Fedha watakaosaidia katika Ulinzi ni VIWAWA Parokia ya Musoma Mjini na Jeshi la Polisi.

Wahusika wote hawa wameombwa kukutana na Mwenyekiti wa Kamati Kuu pamoja na Sekretarieti ya Sinodi siku ya Jumatatu Mei 13. “Nimewaalika tukutane Kanisa Kuu katika Bustani ya Mwenyeheri Yohane Paulo II saa 10 Jioni” alisema Pd. Luvakubandi.

Ni matumaini ya kila mwenye mapenzi mema na Jimbo la Musoma kuwa Ufunguzi wa Sinodi utaashiria mwanzo wa kipindi cha pekee cha neema katika Jimbo.

No comments: